(UTATU MTAKATIFU) KICHOCHEO CHA MAENDELEO TANGANYIKA
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando amesema Ilani ya CCM ya 2015/2020 iko Katika mikono Salama Kwa viongozi wa Wilaya ya Tanganyika kwa kuijenga Tanganyika yenye maendeleo yanayo onekana na kuwagusa moja kwa moja wananchi. Amesema hayo katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Seleman Kakoso na kufanyika katika kijiji cha Majalila wilayani Tanganyika. Mkuu wa Wilaya Mh Salehe Mhando akikabidhiwa Kompyuta na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini kwa niaba ya Kituo cha Polisi Mishamo kilichopo wilayani Tanganyika, ni katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge huyo katika kijiji cha Majalila makabidhiano yamefanyika mara baada ya Mbunge huyo kuhitimisha hotuba yake Katika hotuba ambayo ameitoa mbele ya umati wa wananchi wa jimbo lake ikiwemo kamati ya siasa wilaya ya Tanganyika, na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda amesema Kazi moja kubwa kwa viongozi walio chaguliwa na wananchi ni kutengeneza m...