(UTATU MTAKATIFU) KICHOCHEO CHA MAENDELEO TANGANYIKA



Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando amesema Ilani ya CCM ya 2015/2020 iko Katika mikono Salama Kwa viongozi wa Wilaya ya Tanganyika kwa kuijenga Tanganyika yenye maendeleo  yanayo onekana na kuwagusa moja kwa moja wananchi.

Amesema hayo katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Seleman Kakoso na kufanyika katika kijiji cha Majalila wilayani Tanganyika.


Mkuu wa Wilaya Mh Salehe Mhando akikabidhiwa Kompyuta na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini kwa niaba ya Kituo cha Polisi Mishamo kilichopo wilayani Tanganyika, ni katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge huyo katika kijiji cha Majalila makabidhiano yamefanyika mara baada ya Mbunge huyo kuhitimisha hotuba yake

Katika hotuba ambayo ameitoa mbele ya umati wa wananchi wa jimbo lake ikiwemo kamati ya siasa wilaya ya Tanganyika, na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda amesema Kazi moja kubwa  kwa viongozi  walio  chaguliwa  na wananchi ni kutengeneza mfumo utakaoiunganisha jamii na fulsa za maendeleo.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Mh Seleman Kakoso (wa kwanza kutoka kulia)akikabidhi gari mbili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpanda Mh, Rojas Romul Katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge huyo ambapo gari moja itatumika Katika kusaidia kutembelea Maeneo ya hifadhi za misitu katika wilaya ya Tanganyika ambazo zinamilikiwa na halmashauri, gari la Pili ni Ambulance ndogo itakayo tumika Katika vituo vya afya vya halmashauri ya Mpanda.

Mh Kakoso amekabidhi magari mawili moja likiwa kwaajiri ya kufanyia doria na shughuri mbali mbali za uhifadhi wa misitu katika halmashauri ya Mpanda na nyingine ikiwa ni gari ndogo ya wagonjwa pamoja na  kompyuta 25 zenye thamani ya shiringi milioni 50 kwa shule za sekondari wilayani humo.




Mh Kakoso amekabidhi magari mawili moja  likiwa ni kwaajiri ya kufanyia doria na shughuri mbali mbali za uhifadhi wa misitu katika halmashauri ya Mpanda na lingine ambalo ni aina ya ambulence ndogo ya wagonjwa pamoja na  kompyuta 25 zenye thamani ya shiringi milioni 50 kwa shule za sekondari wilayani humo.












Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.