Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Muhando amesema zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa katika Wilaya yake linaendelea vizuri japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza.
TANGANYIKA:
Mkuu
wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe
Muhando amesema zoezi la
uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa
katika Wilaya yake linaendelea vizuri
japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari amesema zoezi hilo limekumbwa na changamoto ya hali ya mvua kwa baadhi ya
maeneo hasa katika meneo ambayo miundombinu ni mibovu hali iliyopelekea Maafisa
wa Nida kushindwa kufanikisha zoezi hilo.
Aidha amewataka wananchi ambao bado hawajaandikishwa kuendelea kusubiri utaratibu ambao upo chini
ya NIDA.
Zoezi
la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linaendelea katika maeneo mbalimbali
Mkoa wa Katavi hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo.
Comments
Post a Comment