Wakazi wa Kijiji cha Ifukutwa wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya nishati ya Umeme katika eneo hilo. Miundombinu ya umeme katika kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika. Wakizungumza na wandishi wa habari wamesema wameanza kuona faida za nishati ya umeme kutokana na shughuri nyingi kurahisishwa na matumizi ya nishati hiyo. Bi Sarafina,George Abel, Ester Issaick na Kosmas Msumabo wanashukuru kwa uwepo wa umeme katika eneo hilo kwamba umewasaidia kufanikisha shughuri mabali mbali kama vile Saluni, mashine za kusaga na vinywaji baridi. Katika hatua nyingine wameiomba serikali kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme kwenye makazi ya watu kutokana na zoezi hilo awali kulenga maeneo ya huduma za jamii kama vile Shule, vituo vya afya taasisi za kidini na ofisi za umma. Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo amesema serikali inafanya jitihada za dhati kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya Umem...