NEEMA YA UMEME; SERIKALI YAPONGEZWA TANGANYIKA
Wakazi wa Kijiji cha Ifukutwa wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi
wameishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya nishati ya Umeme katika eneo hilo.
Miundombinu ya umeme katika kijiji cha Ifukutwa wilayani Tanganyika. |
Wakizungumza na wandishi wa habari wamesema wameanza kuona faida
za nishati ya umeme kutokana na shughuri nyingi kurahisishwa na matumizi ya nishati
hiyo.
Bi Sarafina,George Abel, Ester Issaick na Kosmas Msumabo wanashukuru kwa uwepo wa umeme katika eneo hilo kwamba umewasaidia kufanikisha shughuri mabali mbali kama vile Saluni, mashine za kusaga na vinywaji baridi.
Katika hatua nyingine wameiomba serikali kuongeza kasi ya
usambazaji wa umeme kwenye makazi ya watu kutokana na zoezi hilo awali kulenga maeneo ya huduma za jamii kama vile Shule,
vituo vya afya taasisi za kidini na ofisi za umma.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo amesema
serikali inafanya jitihada za dhati kuhakikisha wananchi wanapata nishati ya
Umeme ili kuenda sambamba na sera ya taifa ya Viwanda ili kukuza uchumi.
"Lakini pia hii ni fulsa kwa maana vijiji ambavyo vimeunganishwa na huduma ya umeme ni Kabungu, Ifukutwa, Majalila, Kalilankulunkulu na Igalula wananchi wamepokea kwa hamasa zaidi na kuanza kuweka umeme kwenye majumba yao na kuanza kuutumia" alisema Mapengo.
Hapo jana Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk John
Pombe Magufuli wakati akizindua mradi wa umeme wa Kinyerezi ameitaka wizara ya
nishati kupunguza bei ya Umeme ili kila mtanzania apate nishati hiyo kwa
urahisi.
Comments
Post a Comment