Mkuu wa Wilaya yaa Tanganyika Mh: Salehe Mhando atoa shilingi milioni moja kuunga mkono wananchi katika Ujenzi wa shule ya Msingi Luhafwe

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi  Salehe  Mhando ametoa shilingi milioni moja katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa Kijiji cha Luhafwe ambao wameanzisha ujenzi wa vyumba vya madarasa  ya shule ya msingi Ruhafwe iliyopo wilayani Tanganyika.

Mheshimiwa  Salehe Mhando akikagua msingi wa shule hiyo ambao unachimbwa.

Ujenzi huo ambao unatekelezwa na nguvu za wananchi umefikiwa katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Wialaya Salehe  Mhando  kilichofanyika katika kijiji hicho.

Katika mazungumzo yake na wananchi wa Kijiji hicho Mh: Mhando amesema wananchi wameguswa pakubwa na suala la huduma za jamii katika eneo hilo na kujitolea kwa hali na mali huku akieleza kuwa kiasiwa cha shilingi milioni sita tasilimu zimetolewa  na  wananchi hao.

“Niwashukuru sana wananchi wa Luhafwe kwa ushirikiano walio uonyesha katika uanzishwaji wa ujenzi wa hii shule eneo hili la Luhafwe lilikuwa halija rasimishwa na sasa kwa jitihada za halmashauri na serikali kwa ujumla baada ya kulikubali hilo na ndio maana sasa tunakuja na uanzishwaji wa huduma za kijamii “alisema Mhando.

Katika hatua nyingine amesema niwajibu wa kila mwananchi kushiliki katika shughuli za maendeleo ya kijijiji hicho ili kutatua tatizo la ukosefu wa miundo mbinu mbali mbali kama vile afya pamoja na elimu.

DC Mhando ameongeza kusema kuwa serikali ya awamu ya tano kupitia mradi wa Equip imeunga mkono jitihada za wananchi kwa kupeleka kiasi cha Tsh mil 60.5 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa,ofisi moja ya walimu na ujenzi wa vyoo.
Awali eneo hili la Luhafwe halikuwa eneo rasmi la makazi lakin kwa sasa eneo hilo lililopo katika eneo la uwekezaji la halmashauri limerasmishwa rasmi kuwa eneo la makazi.

Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.