Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh.Salehe Mbwana Muhando akizungumza na Wananchi . |
Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na
utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo.
Muhando amebainisha
hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata
ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800
kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Miongoni mwa wananchi Wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando. |
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh.Hamadi Mapengo amesema
mchakato wa kuomba kumiliki msitu huo ulianza mwaka 2002 ambapo kwa sasa kutaongezeka
mapatao yatokanayo na msitu ikiwa ni pamoja na kupata watalii kwa ajili ya kuja
kuwaona wanyama.
Kwa mjibu wa Kaimu wa afisa
ardhi na maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elisha Mengele,vijiji
vipatavyo 11 vinavyozunguka msitu huo vikiwemo Kapanga,Lugonesi,Katuma,Mpembe
na Tongwe vinatarajia kunufaika zaidi na msitu huo.
Comments
Post a Comment