Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando akishiliki katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari hali inayopelekea kushusha kiwango cha ufaulu mkoani katavi. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo salehe muhando wakati wa kipindi cha majadiliano katika kikao cha 11 cha kamati ya ushauri mkoa. Aidha Mh. Mhando amesema uhaba wa shule za kata imekuwa chanzo cha kutengeneza mazingira ya utoro na kuiomba ofisi ya elimu mkoa kuonyesha ushirikiano ktk jitihada zinazotoka kwa wazazi na wilaya hiyo. Wilaya ya Tanganyika iliyopo mkoani katavi ina kata 16 huku ikiwa na shule za kata sekondari 8 pekee.