Wananchi wa kijiji cha Kapanga kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika wametakiwa kuzingatia mpangilio na uboreshaji wa makazi holela ili kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu.





TANGANYIKA
Wananchi wa kijiji cha Kapanga kata ya Katuma wilaya ya Tanganyika wametakiwa kuzingatia mpangilio na uboreshaji wa makazi holela ili kuwasaidia wanafunzi ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu.
Hayo yamesemwa na Afisa mipango miji na vijiji Elisha Mengele wakati akizungumza katika mkutano  na wananchi wa kijiji hicho na kusema kuwa makazi holela yamekuwa ni kikwazo katika sekta ya elimu kwani wanafunzi wamekuwa wakitoka umbali mrefu hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
Naye mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Muhando ametoa rai kwa wananchi ambao wanaishi mbali na huduma za kijamii kuhamia katika maeneo ambayo serikali imetoa kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale ambao wanaishi katika makazi holela.
Kutokana na uwepo wa makazi holela wanafunzi wanaosoma katika shule ya Msingi Kapanga wanalazimika kutembea umbali wa kilomita 30 kila siku.


Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.