Posts

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh.Salehe Mbwana Muhando akizungumza na Wananchi . Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo. Muhando amebainisha hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800 kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. Miongoni mwa wananchi Wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya  ya Tanganyika Salehe Mhando.  Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh.Hamadi Mapengo amesema mchakato wa kuomba kumiliki msitu huo ulianza mwaka 2002 ambapo kwa sasa kutaongezeka mapatao yatokanayo na msitu ikiwa ni pamoja na kupata watalii kwa ajili ya kuja kuwaona wanyama. Kwa mjibu wa Kaimu wa afisa ardhi na maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpand...

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Image
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh:Salehe Mbwana Mhando ambaye alikuwa mgeni lasimi katika fainali ya Ligi ya Mheshimiwa diwani wa Kata ya Tongwe Frenky Kibigasi akikagua timu kabla ya mchezo huo kuanza kati ya timu ya Vikonge na Kalanda mianzi zote za  kutoka kata hiyo. DC Mhando akikagua kikosi cha timu ya Vikonge Fc. DC Mhando akikabidhi kitita kwa mchezaji wa timu ya Vikonge Fc kwa niaba ya timu hiyo ambayo mpaka mchezo unamalizika imeongoza bao 3-1 dhidi Vikonge Fc. DC Mhando AKIWA Katika picha ya Pamoja na timu ya Vikonge Fc ambayo ambayo wamekuwa vinara katika ligi hiyo iliyoshirikisha timu sita zote kutoka katika kata ya Tongwe wilayani Tanganyika.               Mbwewe za mashabiki wa timu ya Kalandamianzi.

(UTATU MTAKATIFU) KICHOCHEO CHA MAENDELEO TANGANYIKA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando amesema Ilani ya CCM ya 2015/2020 iko Katika mikono Salama Kwa viongozi wa Wilaya ya Tanganyika kwa kuijenga Tanganyika yenye maendeleo  yanayo onekana na kuwagusa moja kwa moja wananchi. Amesema hayo katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Seleman Kakoso na kufanyika katika kijiji cha Majalila wilayani Tanganyika. Mkuu wa Wilaya Mh Salehe Mhando akikabidhiwa Kompyuta na Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini kwa niaba ya Kituo cha Polisi Mishamo kilichopo wilayani Tanganyika, ni katika hafla iliyo andaliwa na Mbunge huyo katika kijiji cha Majalila makabidhiano yamefanyika mara baada ya Mbunge huyo kuhitimisha hotuba yake Katika hotuba ambayo ameitoa mbele ya umati wa wananchi wa jimbo lake ikiwemo kamati ya siasa wilaya ya Tanganyika, na madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda amesema Kazi moja kubwa  kwa viongozi  walio  chaguliwa  na wananchi ni kutengeneza m...

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika MH: Salehe Mbwana Mhando amekabidhiwa mifuko ya Saruji 50 yenye thamani ya shiringi milioni 1.

Image
Mkuu  wilaya ya Tanganyika MH:Salehe Mhando akikabidhiwa mifuko ya saruji na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Tumbaku cha Mpanda Kati Nd: Mashaka Shabani Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Mhando akizungumza  na waandishi wa  Habaribaada ya kukabishiwa mifuko hiyo kwaajili ya sekta ya Elimu wilayani Tangayika mkoa wa Katavi pembeni ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda James Rojas Romuli. Nimueendelezo wa Jitihada za DC Mhando kuhamasisha uachangiaji wa hali na mali katika shughuri za maendeleo ya wilaya hiyo kwa sasa ikilenga zaidi kujenga miundo mbinu ya Elimu katika shule za sekondari na shule za msingi wilayani Tanganyika mkoa wa Katavi.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Muhando amesema zoezi la uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa katika Wilaya yake linaendelea vizuri japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza.

Image
TANGANYIKA: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe   Muhando   amesema zoezi la uandikishaji wa   Vitambulisho vya Taifa katika Wilaya yake linaen delea vizuri   japo kuna baadhi ya changamoto ziliweza kujitokeza. Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema zoezi hilo limekumbwa na   changamoto ya hali ya mvua kwa baadhi ya maeneo hasa katika meneo ambayo miundombinu ni mibovu hali iliyopelekea Maafisa wa Nida kushindwa kufanikisha zoezi hilo.      Aidha   amewataka wananchi ambao bado hawajaandikishwa   kuendelea kusubiri utaratibu ambao upo chini ya NIDA. Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa linaendelea katika maeneo mbalimbali Mkoa wa Katavi hivyo wananchi wametakiwa kujitokeza katika zoezi hilo.

KARIBU MWENGE WA UHURU WILAYA YA TANGANYIKA

Image
To

Serikali imetoa milioni 400 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Katika Kata ya Mishamo kilichopo Wilayani Tanganyika.

Image
Aliye valia suti nyeusi ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Mh: Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akiwa na Mkuu wa wilaya Tanganyika Mh: Salehe Mhando wakiwa wakikagua ujenzi wa jengo la kituo cha afya.(PICHA NA DC Mhando ) Serikali imetoa milioni 400 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya Katika Kata ya Mishamo kilichopo Wilayani Tanganyika. Fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi   wodi ya akina mama, na watoto chumba cha upasuaji   maabala pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti na . Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Mbwana Mhando  amesema hayo alipokuwa ameongozana na  Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga katika ukaguzi wa jengo hilo ambalo linaendelea kujengwa.   Jengo la kituo cha  afya Mishamo linalo endelea kujengwa katika wilaya ya Tanganyika (PICHA NA DC Mhando )