Posts

Showing posts from March, 2018

Wakazi wa kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kutatua kero ya maji katika maeneo yao.

Image
TANGANYIKA: Wakazi wa kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika   mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kutatua kero ya maji katika maeneo yao. Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati tofauti na wnananchi hao wamesema kuwa katika maeneo yao suala la maji siyo tatizo hali inayowapa fursa ya kufanya shughuli zingine za kimaendeleo badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji. Kitongoji cha sijonga kimekuwa na utofauti mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine ambayo mkoani Katavi wakazi wake wanalalamika kuwepo kwa kero ya maji. Wiki ya maji Duniani imebeba kauli mbiu Hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii na kwa mkoa wa Katavi imefanyika katika kijiji cha Dilifu.

Halmashauri ya Mpanda mkoa wa Katavi inakadiria kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi na salama Wilayani Tanganyika.

Image
TANGANYIKA NA: Alinanuswe Edward: Halmashauri ya Mpanda mkoa wa Katavi inakadiria kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi na salama Wilayani Tanganyika. Mhandisi wa maji Alkam Omary Sabuni amebainisha hayo mapema leo kupitia Mpanda radio na kuitaja shabaha ya serikali kuwa nikuhakikisha sera ya upatikanaji wa maji vijijini umbali wa mita 400 inatekelezeka kwa vitendo. Katika hatua nyingine ameitaja baadhi ya miradi ya maji ambayo inatumika na wananchi kama sehemu ya mikakati ya halmashauri hiyo kuwa ni mradi wa maji Majalila, Igagala, Ikola na Mishamo.   Wiki hii benki ya dunia imekubali kuisaidia Tanzania kiasi cha dola milioni 300   kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji safi   mijini na vijijini.

Mkuu wa wilaya Mh: Salehe Mhando amekabidhiwa gari kutoka shirika la WaterLid ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya afya na kupambana na maambukizi ya ukimwi wilayani humo.

Image
Gari iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mhando(Picha na DC Mhando) . Mkuu wa wilaya Mh: Salehe Mhando  amekabidhiwa gari kutoka shirika la WaterLid ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya afya na kupambana na maambukizi ya ukimwi wilayani humo. Akizungumza mara baada ya kupokea gari hilo mganga mkuu wa wilaya ya Tanganyika Dk Suleiman Mtenjela amesema gari hilo litasaidia kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya ukimwi kisha kauhidi gari hilo kutumiwa kwa makusudi yaliyotarajiwa Amesema wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile Jografia ya wilaya hiyo na eneo kubwa na vijiji vilivyotawanyika hivyo uwepo wa   gari hilo kutarahisisha kufikika kila mahali Mkuu wa wilaya  ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Mhando aliye valia suti nyeusi na kunyosha mkono juu wenye Funguo za gari alizo kabadhiwa kwa ajiri ya shughuri za kupambana na Maambukizi ya Ukimwi(picha na DC Mhando) Wilaya ya Tanganyika ni wilaya...

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mh : Salehe Mbwana Mhando amewataka Viongozi wa Kata zote za wilaya hiyo, kwa kushirikiana na bodi za shule kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto zilizopo shuleni ili kuinua kiwango cha elimu.

Image
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mbwana Mhando aliye kati kati akisindikizwa na walimu wakati wa ukaguzi wa  miundo mbinu  katika shule ya sekondari Kabungu. TANGANYIKA: Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika   mkoani   Katavi  Mh : Salehe  Mbwana Mhando amewataka Viongozi wa Kata zote za wilaya hiyo, kwa kushirikiana na bodi za shule kuchukua hatua za haraka   kutatua changamoto zilizopo shuleni ili kuinua kiwango cha elimu. Mapema leo amefanya ziara kwa shule za Msingi na shule za sekondari ikiwa na nia ya kukagua maendeleo na uimarishaji wa miundo mbinu katika shule hizo. Wanafunzi wa Shule ya sekonari Kabungu wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando( hayupo pichani) akihimiza kusoma kwa bidii na kueleza mikakati ya serikali awamu ya tano chini ya Dk John Pombe Magufuli katika kuinua sekta ya elimu nchini. Miongoni mwa mambo yaliyo jiri katika ziara hiyo   ni pamoja na suala la utoro ambapo ameagiza bo...

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia tatika wilaya hiyo.

Image
TANGAYIKA: Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia tatika   wilaya hiyo. Akizungumza na Mpanda Radio   amesema agizo lake alilolitoa hivi karibuni akiwataka wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha linaonyesha mafanikio. Aidha amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kupambana na uharifu unaojitokeza huku akiwataka wanaomiliki silaha bila kibali halali kuendelea kuzisalimisha ili kuepuka mkono wa sheria. Wakazi wilayani Tanganyika wanataja miongoni mwa matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za raia nyakati za usiku tangu kuanza mwaka 2018. Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya Salehe Mhando akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalmisha kabla ya msako kuanza baada ya Februari 4 mwaka huu.

Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimechangwa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.

Image
TANGANYIKA: Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimetolewa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu  Raphael Mhuga akihutubia wadau wa Elimu katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa  Idara ya maji mkoani katavi ambapo umefanyika uchangiaji wa  maendeleo ya Elimu katika shule za Sekondari na shule za Msingi wilayani Tanganyika. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhaga ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda Mjini,ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali ili kuleta maendeleo. Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Mh: Salehe Muhando amesema michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa. Mhando ameonya mara kadhaa juu ya uadilifu katika matumizi ya fedha za umma akifafanua kuwa maendeleo hayawezi kuja kama ndoto tu bali uthabiti katika katika kutenda na usimamiaji. ...

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mheshimiwa Salehe Mhando amepokea vifaa mbalimbali kutoka NMB kwa ajili ya kituo cha afya cha Mwese vyenye thamani ya million 5.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mheshimiwa Salehe Mhando amepokea vifaa mbalimbali kutoka NMB kwa ajili ya kituo cha afya cha Mwese vyenye thamani ya million 5. Mheshimiwa Salehe Mhando akipokea vitanda,magodoro,mashine mbili za kupima pressure na seti 3 za vifaa vya kufanyia upasuaji mdogo mdogo. Hizo ni miongoni mwa jitihada zinazofanywa na DC Mhando Katika kuimarisha Huduma ya afya kwa wananchi wa wilaya hiyo. Serikali awamu ya tano chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli imeweka mkazo zaidi katika uimarishaji wa huduma za kijamii ili kama vile afya, ambapo mpango ni kila kata kuwepo na kituo cha Afya.

Mkuu wa mkoa wa katavi meja jenereali mstaafu Rafael Muhuga amewataka wanaume kushirikiana na wanawake katika vita dhidi ya umasikin..

Image
KATAVI.   SIKU YA MWANAMKE DUNIAN. 08/03/2018 Mkuu wa mkoa wa katavi meja jenereali mstaafu Rafael Muhuga amewataka wanaume kushirikiana na wanawake katika vita dhidi ya umasikin.. Kauli hiyo ameitoa katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika kata ya sibwesa wilayan Tanganyika mkoan Katavi Katika hotuba yake Muhuga amesema endapo jamii ikishirikiana kwa pamoja vita hiyo itakuwa imekwisha ndan ya jamii Awali akisoma risala mwenyekiti wa jukwaa LA wanawake wilayan Tanganyika Helen kipoki amesema kuwa wanawake kwa pamoja wamejipanga kupambana na umasikin kwa vitendo baada ya kutekeleza Sera ya Tanzania ya viwanda. Nao baadhi ya wajasiriamali  wanawake waliohudhuria sherehe hizo wamesema kuwa wameiomba serikali kuiwasaidia upatikanaji wa soko ili kurahisisha uuzwaji wa bidhaa wanazozalisha Mkuu wa Wilaya ya Tanganyikamkoani Katavi MH. Salehe Mhando Katika picha akishuhudia burudani mbali mbali Katika maazimisho hayo.  S...

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Salehe Mhando amewaagiza viongozi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma Halmashauri ya wilaya ya mpanda kuwakamata na kuwapeleka mahakamani wazazi wanaowazuia watoto wao kwenda shule.

Image
TANGANYIKA. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Salehe Mhando amewaagiza viongozi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma Halmashauri ya wilaya ya mpanda kuwakamata na kuwapeleka mahakamani wazazi wanaowazuia watoto wao kwenda shule. Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kijiji hicho Mhando amesema zoezi la kuwakamata wazazi hao limeanza tarehe 5 mwezi huu mpaka tarehe 15 amesema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwazuia watoto wao kwenda shule hali ambayo hurudisha nyumba maendeleo ya kitaaluma katika kijiji Kwa upande wa mkurugenzi wa wilaya ya Mpanda Rojaz Lumuli amesema jukumu la kuleta maendeleo katika vijiji ni wajibu wa kila mwananchi kwa kushirikiana na viongozi wao katika nyanja mabalimbali. Kijji cha kamilala kina idadi ya wakazi 1220 ambao wanajihusisha na kilimo na ufugaji shughuli ambazo huwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.

TANGAZO KW A WANANCHI WA MKOA WA KATAVI.

Image
Mh. Salehe Mhando kwa kushilikiana na Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Mpanda Bw. Rojas Romuli John Wanawakukaribisha wadau wote katika kikao cha kuchangia  michango ya kuboresha Elimu Wilayani Tanganyika.

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mh. Salehe Mbwana Mhando anawatangazia wananchi wa Wilaya hiyo Kuhudhuria mkutano wa Wadau wa Elimu.

Image
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika  Mh. Salehe Mbwana Mhando Tarehe 14/3/2018 tutakua na Mkutano wa Wadau wa Elimu Tarafa ya Karema. Mkutano huo utafanyika katika Shule ya Sekondari Karema ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi akuambatana na Katibu Tawala Mkoa, REO, Mkuu wa Wilaya, Viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri. Waalikwa ni Viongozi wa Dini mbali mbali, Walimu wote katika Tarafa, sample ya Wanafunzi, Wazee, Wakuu wa Idara mbali mbali ngazi za Kata, na wote watakaopenda kuja kushiriki akina mam, baba na vijana. Kutakuwa na taarifa za elimu kimkoa, wilaya na kikata. Kutakua na michongo ya hoja katika kukabiliana na changamoto zinazokabili elimu mkoani Katavi hususani Tarafa ya Karema. Mkutano utaanza saa 2:00. Chakula cha mchana kitaandaliwa kwa washiriki wote. Usafiri kufika eneo la tukio itakuwa ni kujitegemea. NAOMBA TUZIDI KUHANASISHANA ILI KUFANIKISHA MALENGO YALIYOKUSUDIWA KATIKA MKUTANO HUO MAHUDHURIO NA KUWAHI  YAUCKIWA NDIO KIPAUMBEKE.

Mkuu wa mkoa wa Katavi ametembelea wilaya ya Tanganyika na kufanya ukaguzi wa mashamba ya Pamba.

Image
Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja jenerali  Mstaafu  Raphael Muhuga kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe  Mhando wakiwa wanaelekea kwenye ukaguzi wa masamba ya Pamba. Mkuu wa mkoa wa Katavi    Meja Jenerali   Mstaafu  Raphael Muhuga  ametembelea  wilaya  ya Tanganyika   na kufanya ukaguzi katika mashamba ya Pamba. Pia amesifia  zao la Pamba kutokana na kustawi vizuri na maendeleo yake ni mazuri. Zao la Pamba katika wilaya ya Tanganyika limeonekana kuendelea kustawi vizuri kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha vizuri.  Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali   Mstaafu  Raphael Muhuga na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando wakiwa katika Shamba la pamba katika Shughuli ya ukaguzi.    Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja Jenerali  Mstaafu  Raphael Muhuga akikagua shamba la Pamba .  Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando aki...