Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi Salehe Mhando amewaagiza viongozi wa kijiji cha Kamilala kata ya Katuma Halmashauri ya wilaya ya mpanda kuwakamata na kuwapeleka mahakamani wazazi wanaowazuia watoto wao kwenda shule.
TANGANYIKA.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika kijiji hicho Mhando amesema zoezi la kuwakamata wazazi hao limeanza tarehe 5 mwezi huu mpaka tarehe 15 amesema kuna baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwazuia watoto wao kwenda shule hali ambayo hurudisha nyumba maendeleo ya kitaaluma katika kijiji
Kwa upande wa mkurugenzi wa wilaya ya Mpanda Rojaz Lumuli amesema jukumu la kuleta maendeleo katika vijiji ni wajibu wa kila mwananchi kwa kushirikiana na viongozi wao katika nyanja mabalimbali.
Kijji cha kamilala kina idadi ya wakazi 1220 ambao wanajihusisha na kilimo na ufugaji shughuli ambazo huwasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.
Comments
Post a Comment