Halmashauri ya Mpanda mkoa wa Katavi inakadiria kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi na salama Wilayani Tanganyika.
TANGANYIKA
NA: Alinanuswe Edward:
Halmashauri ya Mpanda mkoa wa
Katavi inakadiria kuwa ifikapo mwaka 2020 vijiji vingi vitafikiwa na maji safi
na salama Wilayani Tanganyika.
Mhandisi wa maji Alkam Omary
Sabuni amebainisha hayo mapema leo kupitia Mpanda radio na kuitaja shabaha ya
serikali kuwa nikuhakikisha sera ya upatikanaji wa maji vijijini umbali wa mita
400 inatekelezeka kwa vitendo.
Katika hatua nyingine ameitaja
baadhi ya miradi ya maji ambayo inatumika na wananchi kama sehemu ya mikakati
ya halmashauri hiyo kuwa ni mradi wa maji Majalila, Igagala, Ikola na Mishamo.
Wiki hii benki ya dunia imekubali kuisaidia
Tanzania kiasi cha dola milioni 300 kwa
ajili ya ujenzi wa miradi ya maji safi
mijini na vijijini.
Comments
Post a Comment