Mkuu wa mkoa wa Katavi ametembelea wilaya ya Tanganyika na kufanya ukaguzi wa mashamba ya Pamba.




Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja jenerali Mstaafu Raphael Muhuga kushoto akiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe  Mhando wakiwa wanaelekea kwenye ukaguzi wa masamba ya Pamba.

Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja Jenerali  Mstaafu Raphael Muhuga ametembelea wilaya  ya Tanganyika  na kufanya ukaguzi katika mashamba ya Pamba.

Pia amesifia  zao la Pamba kutokana na kustawi vizuri na maendeleo yake ni mazuri.

Zao la Pamba katika wilaya ya Tanganyika limeonekana kuendelea kustawi vizuri kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha vizuri. 

Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali  Mstaafu Raphael Muhuga na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando wakiwa katika Shamba la pamba katika Shughuli ya ukaguzi.  

Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga akikagua shamba la Pamba.

 Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando akiwa anatoa maelekezo kuhusu zao la Pamba.

 Pia Mh. Mhando ameusukuru Mkuu wa mkoa wa Katavi  Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga  na kawataka wakulima waendelee kutuza zao hilo vizuri ili kupata mavuno yaliyo bora na kuwanufaisha wakulima  na familia zao na kukuza kipato katika wilaya ya Tanganyika.

Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.