Mkuu wa wilaya Mh: Salehe Mhando amekabidhiwa gari kutoka shirika la WaterLid ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya afya na kupambana na maambukizi ya ukimwi wilayani humo.

Gari iliyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mhando(Picha na DC Mhando) .

Mkuu wa wilaya Mh: Salehe Mhando  amekabidhiwa gari kutoka shirika la WaterLid ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya afya na kupambana na maambukizi ya ukimwi wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kupokea gari hilo mganga mkuu wa wilaya ya Tanganyika Dk Suleiman Mtenjela amesema gari hilo litasaidia kuboresha huduma na kupunguza maambukizi ya ukimwi kisha kauhidi gari hilo kutumiwa kwa makusudi yaliyotarajiwa


Amesema wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile Jografia ya wilaya hiyo na eneo kubwa na vijiji vilivyotawanyika hivyo uwepo wa  gari hilo kutarahisisha kufikika kila mahali

Mkuu wa wilaya  ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Mhando aliye valia suti nyeusi na kunyosha mkono juu wenye Funguo za gari alizo kabadhiwa kwa ajiri ya shughuri za kupambana na Maambukizi ya Ukimwi(picha na DC Mhando)

Wilaya ya Tanganyika ni wilaya mpya kati ya tatu zinazounda mkoa wa Katavi ikitokana na wilaya ya Mpanda hivyo  huduma nyingi bado zinategemewa kutoka Mpanda Mjini ikiwemo hospitali


Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.