Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Mh : Salehe Mbwana Mhando amewataka Viongozi wa Kata zote za wilaya hiyo, kwa kushirikiana na bodi za shule kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto zilizopo shuleni ili kuinua kiwango cha elimu.


Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mbwana Mhando aliye kati kati akisindikizwa na walimu wakati wa ukaguzi wa  miundo mbinu  katika shule ya sekondari Kabungu.


TANGANYIKA:

Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika  mkoani  Katavi  Mh : Salehe  Mbwana Mhando amewataka Viongozi wa Kata zote za wilaya hiyo, kwa kushirikiana na bodi za shule kuchukua hatua za haraka  kutatua changamoto zilizopo shuleni ili kuinua kiwango cha elimu.

Mapema leo amefanya ziara kwa shule za Msingi na shule za sekondari ikiwa na nia ya kukagua maendeleo na uimarishaji wa miundo mbinu katika shule hizo.

Wanafunzi wa Shule ya sekonari Kabungu wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Salehe Mhando( hayupo pichani) akihimiza kusoma kwa bidii na kueleza mikakati ya serikali awamu ya tano chini ya Dk John Pombe Magufuli katika kuinua sekta ya elimu nchini.

Miongoni mwa mambo yaliyo jiri katika ziara hiyo  ni pamoja na suala la utoro ambapo ameagiza bodi za shule kwa kushirikiana na Wazazi na Walezi kuhakikisha wana komesha vitendo hivyo ambavyo amevitaja kuwa kikwazo  cha ukuaji wa elimu katika wilaya hiyo.

Katiki hatua nyingine ameagiza kukamatwa kwa wazazi wote ambao wanachangia kuwepo kwa utoro kwa wanafunzi kutokana na kuwatumikisha mashambani.


Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando akiwa shule ya msingi Igalula wakati wa kutembelea shule za msingi na sekondari ziara iliyo lenga kuhimiza uwajibikaji kwa bodi za shule na viongozi wa kata katika kuchochea ukuaji wa taaluma wilayani humo.

Wiki iliyopita wadau wa elimu Mkoani Katavi wamechangia zaidi ya milioni 150 kwaajili ya kuimarisha miundo mbinu ya elimu wilayani Tanganyika.

Comments

Popular posts from this blog

MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA MKOA WA KATAVI DC SALEHE MHANDO ASEMA MAPAMBANO DHIDI YA UVUVI HARAMU NI ENDELEVU

Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Muhando akabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa kwanza mpaka msihindi wa tatu katika ligi ya kata ya Tongwe wilayani Tanganyika na kuwataka vijana kuunganishwa na dhamila ya Uzalendo na maendeleo kupitia michezo.

Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari.