Zaidi ya Shilingi milioni 152 zimechangwa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.
TANGANYIKA:
Zaidi ya
Shilingi milioni 152 zimetolewa na wadau wa elimu wilayani Tanganyika,ili kutatua
matatizo ya miundombinu ya elimu wilayani humo.
Mkuu wa
Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhaga ambaye alikuwa mgeni rasmi
katika hafla hiyo ambayo imefanyika Mpanda Mjini,ametoa wito kwa wadau wengine kuendelea
kushirikiana na serikali ili kuleta maendeleo.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Tangayika Mh: Salehe Muhando amesema
michango yote iliyopatikana lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa.
Mhando ameonya mara
kadhaa juu ya uadilifu katika matumizi ya fedha za umma akifafanua kuwa
maendeleo hayawezi kuja kama ndoto tu bali uthabiti katika katika kutenda na
usimamiaji.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mheshimiwa Salehe Mhando akizungumza mbele ya wadau wa Elimu katika ukumbi wa Idala ya Maji mkoani Katavi.
Naye Mbunge
wa jimbo la Mpanda vijijini Mh.Suleimani Kakoso amechangia komputa kwa
shule za sekondari,vifaa vya ujenzi na fedha taslimu, nakuzishauri halmashauri
Mkoani Katavi kuwashirikisha wadau wa maendeleo walioko ndani na nje ya
halmashauri zao ili washiriki kuleta maendeleo katika elimu na nyanja mbali mbali.
Wadau wa
elimu ambao wameshiriki wanatoka taasisi za kifedha,wafanyabiashara,madiwani
halmashauri ya wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara wilayani Tanganyika,wakulima,
pamoja na watu binafsi.
Wadau wa elimu wakifuatilia kwa umakini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga
BAADHI YA VITU AMABYO VIMECHANGWA
KOMPUTA 24 Zeny thamani y ash.mil.48
MIFUKO YA SIMENTI MIFUKO 2281-Sh.milioin 41,058,000
VITANDA DABODEKA 25-….SH.MIL 5,000,000
Malumalu box 200- sh.mil.5
Bando za bati 1530---Mil.30,400,000
Fedha taslimu-sh.400,000
Fedha ahadi Sh.Mil 17,400,000
Kokoto kubwa Tan 14—Sh.520,000
Kokoto Vumbi tan 14-Sh.160,000
Mpango huu unatalajiwa kuleta tija kwa ustawi wa elimu katika wilaya hiyo yenye takribani kata 15
Comments
Post a Comment