Mh. Salehe Mhando kwa kushilikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda Bw. Rojas Romuli John Wanawakukaribisha wadau wote katika kikao cha kuchangia michango ya kuboresha Elimu Wilayani Tanganyika.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh:Salehe Mbwana Mhando aliye kati kati akiwa katika operesheni ya kuchoma nyavu haramu zinazotumika ziwa Tanganyika lilipopo wilayani Tanganyika mkoani Katavi kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh:Hamadi Mapengo. Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh: Salehe Mbwana Mhando akishuhudia uchomaji wa nyavu zisizo faa katika uvuvi katika mwambao wa ziwa Tanganyika eneo la Ikola na Kalema.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh:Salehe Mbwana Mhando ambaye alikuwa mgeni lasimi katika fainali ya Ligi ya Mheshimiwa diwani wa Kata ya Tongwe Frenky Kibigasi akikagua timu kabla ya mchezo huo kuanza kati ya timu ya Vikonge na Kalanda mianzi zote za kutoka kata hiyo. DC Mhando akikagua kikosi cha timu ya Vikonge Fc. DC Mhando akikabidhi kitita kwa mchezaji wa timu ya Vikonge Fc kwa niaba ya timu hiyo ambayo mpaka mchezo unamalizika imeongoza bao 3-1 dhidi Vikonge Fc. DC Mhando AKIWA Katika picha ya Pamoja na timu ya Vikonge Fc ambayo ambayo wamekuwa vinara katika ligi hiyo iliyoshirikisha timu sita zote kutoka katika kata ya Tongwe wilayani Tanganyika. Mbwewe za mashabiki wa timu ya Kalandamianzi.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh. Salehe Mhando akishiliki katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za sekondari hali inayopelekea kushusha kiwango cha ufaulu mkoani katavi. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo salehe muhando wakati wa kipindi cha majadiliano katika kikao cha 11 cha kamati ya ushauri mkoa. Aidha Mh. Mhando amesema uhaba wa shule za kata imekuwa chanzo cha kutengeneza mazingira ya utoro na kuiomba ofisi ya elimu mkoa kuonyesha ushirikiano ktk jitihada zinazotoka kwa wazazi na wilaya hiyo. Wilaya ya Tanganyika iliyopo mkoani katavi ina kata 16 huku ikiwa na shule za kata sekondari 8 pekee.
Comments
Post a Comment