Wakazi wa kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi wameipongeza serikali kwa kutatua kero ya maji katika maeneo yao.
TANGANYIKA:
Wakazi wa kitongoji cha Sijonga kata ya Kabungu
wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi
wameipongeza serikali kwa kutatua kero ya maji katika maeneo yao.
Wakizungumza na Mpanda Redio kwa nyakati
tofauti na wnananchi hao wamesema kuwa katika maeneo yao suala la maji siyo
tatizo hali inayowapa fursa ya kufanya shughuli zingine za kimaendeleo badala
ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Kitongoji cha sijonga kimekuwa na utofauti
mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine ambayo mkoani Katavi wakazi wake
wanalalamika kuwepo kwa kero ya maji.
Wiki ya maji Duniani imebeba kauli mbiu
Hifadhi maji na mfumo wa kiikolojia kwa maendeleo ya jamii na kwa mkoa wa
Katavi imefanyika katika kijiji cha Dilifu.
Comments
Post a Comment