Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia tatika wilaya hiyo.
TANGAYIKA:
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe
Mhando amesema,vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo vinaendelea kuwasaka
na kuwakamata waharifu mbalimbali wanaohatarisha usalama wa raia tatika wilaya hiyo.
Akizungumza na Mpanda Radio amesema agizo lake alilolitoa hivi karibuni akiwataka
wanaomiliki silaha kinyume na sheria kuzisalimisha linaonyesha mafanikio.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano
kwa jeshi la polisi ili kupambana na uharifu unaojitokeza huku akiwataka
wanaomiliki silaha bila kibali halali kuendelea kuzisalimisha ili kuepuka mkono
wa sheria.
Wakazi wilayani Tanganyika wanataja miongoni mwa
matukio yanayotokea mbali na mauaji kuwa ni uporaji wa mali za raia nyakati za
usiku tangu kuanza mwaka 2018.
Januari 22 mwaka huu,mkuu wa Wilaya Salehe Mhando
akiwa ziarani kata ya Kasekese alitoa agizo kwa wanaomiliki silaha kinyume na
sheria kuzisalmisha kabla ya msako kuanza baada ya Februari 4 mwaka huu.
Comments
Post a Comment