Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mh.Salehe Mbwana Muhando akizungumza na Wananchi . Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Mh: Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo. Muhando amebainisha hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800 kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo. Miongoni mwa wananchi Wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Salehe Mhando. Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh.Hamadi Mapengo amesema mchakato wa kuomba kumiliki msitu huo ulianza mwaka 2002 ambapo kwa sasa kutaongezeka mapatao yatokanayo na msitu ikiwa ni pamoja na kupata watalii kwa ajili ya kuja kuwaona wanyama. Kwa mjibu wa Kaimu wa afisa ardhi na maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpand...